Wakazi wa Arusha wakiwa wamejitokeza kwaajili ya kuchukua fomu za ushiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents litakaloanza Rasmi Kesho katika Ukumbi wa Tripple A, Arusha.Zoezi la kuchukua fomu litaendelea kwa siku mbili hadi hapo Jumatatu.
Mshiriki Kutoka Mkoani Mwanza ambae alishiriki katika shindano la Tanzania Movie Talents katika Kanda ya Ziwa, mkoani Mwanza na kutobahatika Kushinda akijaza fomu yake kwaajili ya kujaribu tena bahati yake katika Shindano la Tanzania Movie Talents litakaloanza kesho katika Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha
Timu ya Tanzania Movie Talents ikiwa tayari kwaajili ya kuwapa washiriki fomu za kushiriki shindano la Tanzania Movie Talents kwa washiriki watakaojitokeza kwa siku ya leo.
Vijana Wa Tanzania Movie Talents (TMT) wakiweka tear drop nje ya ukumbi wa Tripple A, Jijini Arusha Mapema leo.
Mpita njia Akisoma tear drop ya Tanzania Movie Talents (TMT) wakati akipita pembeni ya barabara kuu ya Nairobi Arusha leo.
Mc Pilipili (Kulia) akiwa na Dada Happy wakiwatangazia Umma wa Watanzania waishio Kanda ya Kaskazini Mkoa wa Arusha Juu ya Kuweza kujitokeza kwaajili ya Kushiriki Katika Shindano la Tanzania Movie Talents litakaloanza rasmi kesho na hatimaye kuwezesha washindi watatu kuzawadiwa Zawadi zao za Kitita cha Shilingi laki tano kila Mmoja.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)