
URENO imetaja kikosi chake cha
awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya kombe la dunia mwezi ujao nchini
Brazil, huku nyota wa Real Madrid na mwanasoka bora wa dunia, Cristiano
Ronaldo akiongoza jahazi.
Ronaldo na Ureno yake wapo kundi
moja na Ujerumani, Marekani na USA na wataanza kampeni zao za kusaka
ubingwa dhidi ya Ujerumani juni 16 mwaka huu. Kocha mkuu Paulo Bento ametaja kikosi cha awali cha wacheza 30 kitakachopunguzwa mpaka kufikia 23 tayari kwa safari ya Brazil.
Ronaldo ameitwa pamoja na nyota wenzake wa Real Madrid, Simon Pepe na Fabio Coentrao.
Wakati huo huo mchezaji wa Porto, Ricardo Quaresma amejumuishwa baada ya kureja katika klabu yake ya zamani mapema msimu huu.
Kusoma zaidi bofya kikosi cha Ureno bofya www.bkmtata.blogspot.com





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)