Msanii Lucas Mhavile ‘Joti’baada ya kukaa kimya kwa muda sasa ameibuka na filamu yake ya Joti Sanduku la Babu ambayo amecheza katika uhusika tofauti tofauti filamu hiyo itakuwa ikisambazwa na Kampuni ya Proin Promotions ya jijini Dar es salaam
Akizungumzia filamu hiyo Joti alisema kuwa amekuja kivingine kwani kitu alichofanya katika filamu hiyo haijawai kutokea wala kufanywa na mtu yoyote yule katika tasnia hii ya filamu nchini, hivyo wapenzi wangu wakae mkao wa kula tu kwani wakati wowote kuanzia sasa itakuwa inaingia sokoni kwani filamu hii si yakukosa maana unambiwa uzee mwisho chalinze mjini kila mtu honey
Hivyo wapenzi wa filamu nawaomba wanunue nakala halisi ya filamu hiyo pindi itakapotoka ambapo nimeelezea mambo mbalimbali ya ujana usichana pamoja na uzee, mbali na hivyo filamu hiyo imebeba mambo matatu muhimu kwanza ina burudisha pia ina elimisha na kupata ujumbe muhimu kabisa katika jamii inayotuzunguka.Filamu hiyo ya kwanza tangu joti aweke kando mambo ya filamu na kujiingiza katika mambo ya uchekeshaji kupitia runinga sasa amerudi tena katika filamu yake mwenyewe inayokwenda kwa jina la joti sanduku la babu





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)