NAY WA MITEGO - WIMBO WANGU WA "NAKULA UJANA UNANIFURAHISHA" - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NAY WA MITEGO - WIMBO WANGU WA "NAKULA UJANA UNANIFURAHISHA"

Msanii Ney wa Mitego pichani.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MWIMBAJI wa Hip Hop, Emmanuel Elbariki maarufu kama Ney wa Mitego, amesema wimbo wake wa ‘Nakula Ujana’ unampa raha kutokana na kupokewa  kwa shangwe na mashabiki wa kizazi kipya nchini.



Ney wa Mitego aliyasema hayo katika mazungumzo ya kuelezea namna gani amejiwekea mikakati ya kulinda hadhi na uwezo wake kisanaa jijini Dar es Salaam.


Alisema kuwa wimbo wake huo wa Nakula Ujana umetokea kupendwa
na wengi, hasa anapokuwa katika maonyesho mbalimbali, hivyo kuonyesha kuwa maendeleo yake kisanaa yamekuwa mazuri kupita kiasi.



“Nawashukuru wadau wangu wote kwakuwa wanapenda kazi zangu, hasa huu wimbo wa Nakula Ujana, ambao mimi mwenye unanipa raha. “Naamini kila kitu kitakuwa kizuri zaidi kwa kuwapatia raha  mashabiki wangu wakati wowote, kwakuwa bado nitaendelea kupambana ili kufanya vizuri zaidi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages