KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA USAFIRI WA ANGA (ICAO) BW,RAYMOND BENJAMIN AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA USAFIRI WA ANGA (ICAO) BW,RAYMOND BENJAMIN AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,kwa ziara ya kikazi nchini kuanzia leo tarehe 14 hadi 18 Mei 2014. Tanzania ni moja ya nchi mbili ikiwemo Ethiopia atakazotembelea katika Kanda ya ICAO .
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe watatu kutoka (kushoto) akiwa na wakurugenzi na Wakuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCCA) wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin wakati walipokuwa wakibadilishana mawazo baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi kuanzia leo tarehe 14 hadi 18 Mei 2014.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin( Kulia) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ziara ya Kikazi hapa nchini.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe wapili kutoka kushoto akiongea wakati alipokuwa akimkaribisha Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin watatu kutoka (kushoto)baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,kwa ziara ya kikazi nchini kuanzia leo tarehe 14 hadi 18 Mei 2014. Tanzania ni moja ya nchi mbili ikiwemo Ethiopia atakazotembelea katika Kanda ya ICAO .
Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin wa tatu kutoka (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe na Viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages