JAJI SINGLE MTAMBALIKE AELEKEA JIJINI DAR KWAAJILI YA KUHUDHURIA MAZISHI YA MAREHEMU ADAM KUAMBIANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JAJI SINGLE MTAMBALIKE AELEKEA JIJINI DAR KWAAJILI YA KUHUDHURIA MAZISHI YA MAREHEMU ADAM KUAMBIANA

Jaji wa Mashindano ya Tanzania Movie Talents , Single Mtambalike almaarufu kama Rich Rich akipanda kwenye ndege kutoka Jijini Arusha kuelekea Dar Es Salaam kwaajili ya kuhudhuria Mazishi ya Msanii na Muongozaji wa Filamu Tanzania Marehemu Adama Kuambiana. 

Ni Ngumu kwa timu nzima ya Tanzania Movie Talents iliyopo Mkoani Arusha kwaajili ya kazi ya kusaka vipaji vya Kuigiza kuelekea Mkoani Dar Kwaajili ya Mazishi lakini Timu nzima imemteua Jaji Rich Kuhudhuria Mazishi hayo ikiwa anaiwakilisha Timu Nzima ya Tanzania Movie Talents.

Tanzania Movie Talents tunatambua mchango wa Msanii Adam Kuambiana imeamua kusitisha zoezi kwa siku ya leo na Kuungana na Watanzania Katika Msiba Huu Mkubwa katika Tasnia ya Filamu Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages