
KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka imepanga kutumia vyombo vipya vya muziki katika Tamasha la Pasaka, Mei 4 jijini Mwanza.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama hivi sasa kamati yake bado inaendelea na taratibu za kuvileta vyombo hivyo.
Msama alisema vyombo hivyo vya kisasa wameviagiza nchini China ambavyo ni vya kisasa zaidi katika tasnia ya muziki duniani.Aidha Msama alisema sababu za kuagiza vyombo hivyo vipya ni kuwasaidia wanamuziki wetu kuachana na mtindo wa kutumia CD katika matamasha na badala yake wanatakiwa kuimba ‘live’.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)