Kata ya Pera; Malivundo Ofisi ya Mtendaji; CCM 77, CHADEMA 2, CUF , AFP 1, NRA 1.
Kimbugi; CCM 11, CHADEMA 1, CUF 0, AFP 0, NRA 0
Magange Ofisi ya Kitongoji; CCM 101, CHADEMA 1, NRA 0, AFP 0
Pingo Shule ya Msingi Namba 1; CCM 31, CHADEMA 1, CUF 1, NRA 0, AFP 0
Pingo Ofisi ya Kitongoji Namba 2; CCM 61, CHADEMA 4, CUF 2, AFP 1, NRA 0
Pingo Namba 1; CCM 66, CHADEMA 0, NRA 0, AFP 0
- Matokeo ya awali kwa baadhi ya vituo yanaonesha kuwa mgombea wa CCM Ridhiwani Kikwete anaongoza kwa kiasi kikubwa.
- Kazi ya kuhesabu kura katika Jimbo la Chalinze imeanza na matokeo yatatangazwa muda wowote kuanzia sasa.
- Baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani ikiwa ni pamoja na CHADEMA wamelalamikia mwenendo wa uchaguzi wa ubunge Jimboni Chalinze.
- Rais Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wamejitokeza kupiga kura katika kituo cha shule ya Msingi Msoga kuchagua mbunge wa Chalinze.
- Wakazi wa jimbo la Chalinze wamejitokea kwa wingi kupiga kura kumchagua mbunge wao. Zoezi limemalizika kwa amani na utulivu.
Wakati huo Kurugenzi ya Habari CHADEMA imeelezea HALI ILIVYOKUWA NA MATOKEO YA AWALI CHALINZE kama ifuatavyo:-
Uchaguzi wa mdogo wa Jimbo la Chalinze umefanyika huku ukigubikwa na kasoro kadhaa, ikiwa ni pamoja na watu wachache kujitokeza vituoni kupiga kura, wapiga kura kulalamika ‘kupokwa’ vitambulisho vyao, vituo kuwa majumbani kwa watu, huku pia kukiwa na hofu ya vurugu.
Kasoro hizo zilijidhihirisha jana wakati wapiga kura shughuli ya upigaji kura ilipokuwa ikiendelea katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo ambapo wananchi wa Chalinze walikuwa wakipiga kura mbunge wao, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Said Bwanamdogo aliyefariki mapema mwaka huu.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)