MKOA WA DODOMA WASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA NCHINI MKOANI DODOMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKOA WA DODOMA WASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA NCHINI MKOANI DODOMA

 Mkuu wa Mkoa  Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akifanya ukaguzi wa vitabu na nyaraka za taarifa mbalimbali  kwa ajili ya wasomaji , pembeni yake ni Mkutubi msaidizi wa maktabaa hiyo Ndg. Judith Lugongo, ukaguzi huo ulifanyika mapema Leo hii wakati wa  maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba mkoa wa Dodoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye  kilemba kichwani) akikagua jengo la maktaba mkoa wa Dodoma kujionea  mfumo wa vifaa vinavyotumika kutolea elimu na taarifa mbalimbali kwa  njia ya video na sauti,  zoezi hili la ukaguzi lilifanyika mapema leo
kwenye viwanja vya maktaba ya Dodoma wakati wa maadhimisho  ya miaka 50 ya  bodi ya huduma za maktaba
 Watumishi wa maktaba ya mkoa Dodoma wakiwa tayari kupokea wananchi wenye mahitaji mbalimbali ya huduma za maktaba kwa  ajili ya kuwapa maelekezo ya namna ya kupata taarifa na huduma nyingine  mbalimbali mapema leo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya  huduma za maktaba, maadhimisho mkoa Dodoma yalifanyika viwanja vya  maktaba ya Dodoma.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akikagua nyaraka na vitabu  mbalimbali wakati akitembelea mabanda ya maonesho  ya vitabu wakati wa  maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba Nchini, maadhimisho mkoa Dodoma yalifanyika viwanja vya maktaba ya mkoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye  kilemba kichwani) akipata ufafanuzi kutoka kwa mtaalamu wa kutafsiri  taarifa za vitabu na nyaraka mbalimbali katika lugha za watu wenye  mahitaji maalumu/wenye ulemavu wa kuona (nukta nundu) Mwl. Charles  Mtimatuku mapema wakati anatembelea mabanda ya maonesho wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba nchini  mkoani Dodoma. Huduma za maktaba nchini zimepiga hatua kiasi cha  kuzalisha taarifa na nyaraka mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Baadhi ya walimu na wanafunzi shule za Dodoma  waliojitokeza kwenye viwanja vya maktaba ya mkoa Dodoma kushiriki maadhimisho  ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba nchini wakifuatilia salamu za  mkuu wa mkoa Dodoma mapema leo.


Picha NA JOHN BANDA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages