Majaji wa Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents, Single Mtambalike (kulia), Yvonne Chery (Katikati) na Roy Sarungi.
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza
Hatimaye shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lakaribia kufika ukingoni baada ya kazi nzito na kubwa ya majaji kuhakikisha wanachagua mtu anayestahili na mwenye kipaji.
Zoezi zima la Kujaji washiriki lilikua likiendeshwa na Majaji wa tatu ambao ni Single Mtambalike, Yvonne Cherry na Roy Sarungi ambao Muda si mrefu watawatangaza washindi watatu ambao wataibuka na kitita cha Shilingi laki 5 kila mmoja na hatimaye kujumuika na washindi wengine watatu kutoka kila kanda ambao watashindana katika Fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na Mshindi kujishindia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Shindano hili litafanyika kikanda nchini Nzima ambapo kwenye kila Kanda watapatikana washindi watatu ambao Watajumuika pamoja katika Fainali itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na kupelekea Mshindi kuibuka na Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania
Shindano hili ni la kwanza kufanyika nchini Tanzania na Afrika Mashariki na Kati ambao shindano hili limeanzia kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza ambapo muda si mrefu majaji watawatangaza washindi wa Mkoani Mwanza ambapo unawakilisha Kanda ya ziwa.
Washiriki walikuwa wengi na wengi waliweza kuonyesha Vipaji vyao lakini kwenye Mashindano Kuna Kushinda na kushindwa lakini pia Washiriki ambao hawajapata bahati ya kuwa washindi watatu sio kwamba hawana uwezo, uwezo wanao na hakika wameweza kuonyesha Vipaji vyao.
Baada ya Mashindano haya kumalizika kanda ya ziwa Mkoani Mwanza , Shindano hili litahamia Kanda ya Kati, Mkoani Dodoma ambapo watanzania wanaojihisi wanavipaji wanashauriwa kujitokeza kwa wingi mkoani Dodoma kwaajili ya Kuonyesha Vipaji.
Fomu za kujiunga ni bure kabisa na hakuna malipo yoyote yale yanayotakiwa kulipwa kwaajili ya kuchukua fomu.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)