Uzinduzi wa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2014 utafanyika siku ya Alhamisi tarehe 20 Machi 2014 saa 5.00 kamili asubuhi katika hotel ya JB Belmont ukumbi wa Savannah jijini Dar es salaam.
Awali uzinduzi huu ulikuwa ufanyike sambamba na semina ya mawakala, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, imebidi semina isogezwe mbele hadi tarehe 25 Machi 2014.
Mawakala waliopo jijini Dar es salaam na wale wenye nafasi mnakaribishwa kuhudhuria uzinduzi huu.
Natanguliza shukrani.
HIDAN .O. RICCO.
PRO Redds Miss Tanzania





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)