SIKU YA KUMI NA MOJA BAADA YA NDEGE KUPOTEA: NDUGU WA ABIRIA WA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA WAISHUTUMU SERIKALI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SIKU YA KUMI NA MOJA BAADA YA NDEGE KUPOTEA: NDUGU WA ABIRIA WA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA WAISHUTUMU SERIKALI

Wanawake wawili (mmoja hayupo pichani) wakiondolewa kwa nguvu kwenye mkutano wa waandishi wa habari ambao ulipangwa kufanyika leo mjini Kuala Lumpur.  Wanawake hao ni baadhi ya ndugu ‘waliopotea’ katika ndege aina ya Boeing 777 namba MH370 iliyopotea zaidi ya siku 10 zilizopita ambao wameilaumu serikali ya Malaysia kwa kutowaambia ukweli na kuwazungusha kuhusu juhudi za kweli kuhusiana na ndugu zao.
Mmoja wa wanafamilia walipotelewa ndugu akiongea kwauchungu na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.
Mwanamke akiondolewa na maofisa usalama wakati alipojaribu kulalamika kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika hoteli ya Sepang mjini Kuala Lumpur.
Familia ya Wachina waliokuwa na ndugu katika ndege ya Malaysia, wakisindikizwa kutoka kwenye mkutano wa waandishi wa habari.
Moja ya ndege za Jeshi la Maji la Marekani ikitayarishwa kwenda kuisaka ndege ya Malaysia iliyopotea.
Ndege nyingine ya jeshi la Marekani ikisafishwa ili kwenda kuitafuta ndege ya Boeing 777 iliyopotea. CHANZO: DAILYMAILY

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages