Muigizaji wa Filamu za Kitanzania Single Mtambalike almaarufu Rich Rich ambae pia ni mmoja wa majaji katika Shindano la kusaka vipaji vya uigizaji lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lililopo chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited akiongelea jinsi washindi watakavyopatikana katika shindano hilo linalotarajia kuanza tarehe 1 Aprili 2014
..............................................................
Mwigizaji mkongwe nchini na anayesifika kwa kutokuwa na skendo za hapa na pale kama wasanii wengine Single Mtambalike maarufu kama “Richie” amesema kuwa vyombo vingi vya habari nchini vinamkimbia na kukwepa kuandika habari zake kwakuwa yeye hapendi habari za skendo ili mradi tu asikike ndio maana imekuwa nadra sana kumskia akiandikwa kwenye mitandao na magazeti.
Richie aliyazungumza hayo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kusaka vipaji nchini toka kampuni ya filamu ya Proin Promotions. Richie alisema kuwa vyombo vingi vya habari vinapenda kuwafuatilia sana waigizaji wenye skendo hasa za mapenzi kwani habari hizo ndio zinauza sana na kupendwa kusomwa na watu wengi na kuacha kuandika mambo ya maana yatakayoijenga tasnia ya filamu nchini.
Richie alitilia mkazo kwa waandishi wa magazeti, blogs na vyombo vingine vya habari kuwa kama kweli wanataka kukuza Sanaa hii ya filamu nchini, basi hawana budi kuepukana na kasumba hiyo na kuandika mambo yenye maana.
Richie atakuwa mmoja wa majaji katika shindano hilo la kusaka vipaji nchini litakalojulikana kama Tanzania Movie Talent.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)