Meneja wa Huduma kwa wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Godfrey Mollel akisisitiza jambo wakati akitoa mada kwenye mkutano ulioandaliwa na PPF kwa waandishi na wadau wa habari katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam.Picha na Maktaba
Stori: Mwandishi Wetu
MFUKO wa Pensheni (PPF) umesema kwamba endapo waajiri wa sekta mbalimbali waliojiunga na mfuko huo watashindwa kuwakilisha michango ya wafanyakazi wao kwa muda unaotakiwa hawatasita kuwachukulia hatua.
Kauli hiyo ilitolewa na Meneja Huduma kwa Wanachama wa PPF, Godfrey Mollel wakati alipokuwa akitoa mada juu ya kujiunga na mfuko huo na faida zake katika mkutano wa mwaka wa waandishi na wadau wa habari uliofanyika wiki iliyopita katika Ukumbi wa Karimjee jiini Dar es Salam.
Meneja huyo alifafanua kuwa kuna baadhi ya waajiri ambao wafanyazi wao ni wanachama lakini wamekuwa wakichelewa kuwakilisha michango ya wafanyakazi wao.
“Tutakuwa tunawakumbusha kwanza bila kuwachukulia hatua lakini pale inaposhindikana ndipo tutafikia hatua hiyo ya kuangalia njia nyingine ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani,” akisema Mollel.
Hata hivyo, amewataka waajiri ambao bado hawajajiunga, wajiunge pamoja na wafanyakazi wao au mjasiriamali nao wanaweza kujiunga na mfuko huo.
Awali mkutano huo ulifunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PPF, William Erio (pichani) na ulihudhuriwa na waandishi na wadau wa habari 130 ambapo watu 90 walijiunga na mfuko huo siku ya tukio.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)