NEWS ALERT: MISSING MALYSIAN JET: Picha ya 'mabaki ya ndege' iliyopotea - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NEWS ALERT: MISSING MALYSIAN JET: Picha ya 'mabaki ya ndege' iliyopotea


China imeanza kuchunguza picha mpya za setilite zinazoonyesha kitu kama mabaki ya ndege kwenye eneo la kusini mwa bahari ya Hindi.
Picha hizo ni muhimu kwa ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea, maafisa wa Malaysia wanasema.
Kaimu Waziri wa Usafirishaji Hishammuddin Hussein amesoma taarifa hiyo baada ya kukabidhiwa ambapo amesema kuna kitu kama mabaki ya ndege chenye ukubwa wa mita 30 kwa 22 kilichoonekana.
Amesema serikali ya China itaendelea kutoa taarifa zaidi hapo baadae.
Ndege MH370 mali ya Shirika la ndege la Malaysia ilipotea kwenye masiliano ilipokuwa imeondoka kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing march 8 ikiwa na abiria 239.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages