Mtoto wa Rais Jakaya Kikwete,Ndugu Ridhiwani Kikwete akijipigia kura.
Leo kumefanyika Upigaji Kura za maoni kupitia chama cha CCM,jimbo la Chalinze,aidha Katika uchaguzi huo uliofanyika Ridhiwani Kikwete amishinda kwa kuibuka na kura 758 kati ya kura 1321 zilizopigwa, huku mpinzani wake wa karibu ambaye pia ni mdau mkubwa wa Soka hapa nchini,Ndugu Shaban Iman Madega ameibuka na kura 335.
Wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni pamoja na Athuman Ramadhan Maneno aliyepata kura 206 na Changwa Mohamed Mkwazu aliyeambulia kura 12.
Katika uchaguzi huo jumla ya kura zote zilikuwa ni 1363 wakati kura zilizoharibika ni 5 na Halali ni kura 1316, hivyo kwa matokeo hayo Kikwete anasubiri vikao vya juu vya chama ili kutoa baraka kama ateuliwe kuwa mgombea ama vinginevyo.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)