MADEREVA BODABODA, BAJAJ WAANDAMANA KUPINGA KUZUIWA KUINGIA KATIKATI YA JIJI LA DAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MADEREVA BODABODA, BAJAJ WAANDAMANA KUPINGA KUZUIWA KUINGIA KATIKATI YA JIJI LA DAR

Madereva Bajaj na bodaboda wakiwa nje ya ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar wakipinga tamko la kuzuiwa kuingia katikati ya jiji.Polisi wakiwa eneo la tukio kudumisha ulinzi.
Mmoja wa madereva Bajaj akiongea na vyombo vya habari nje ya ofisi za Chadema.
WAENDESHA bodaboda na Bajaj jijini Dar leo wameandamana mpaka ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zilizopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Nia ya maandamano hayo ni kupinga tamko linalowataka kutopeleka abiria maeneo yote ya katikati ya jiji la Dar.
Mmoja wa madereva hao, akiongea na wanahabari alisema kwamba wameamua kuandamana mpaka ofisi za Chadema kwa kuwa wanaamini ndio watapata msaada wa tatizo lao.
(HABARI NA DJ SEK BLOG)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages