MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KITAIFA YAENDELEA MKOANI DODOMA,MKUU WA MKOA WA DODOMA DR REHEMA NCHIMBI AMEZINDUA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA CHIDIDIMO MANISPAA YA DODOMA(18/3/2014) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KITAIFA YAENDELEA MKOANI DODOMA,MKUU WA MKOA WA DODOMA DR REHEMA NCHIMBI AMEZINDUA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA CHIDIDIMO MANISPAA YA DODOMA(18/3/2014)

 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi  akisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi Chididimo waliojitokeza kumlaki alipowasili kijijini hapo kuzindua mradi wa maji kijijini hapo,  mapema leo hii.
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi(kushoto) akipokea taarifa ya mradi wa maji kijiji cha  Chididimo manispaa ya Dodoma kama inavyowasilishwa kwake na mhandisi
Mohamed Khali ( Kulia)  kutoka idara ya maji manispaa ya Dodoma  wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika leo.
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi  akizindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Chididimo manispaa ya Dodoma leo, wengine ni wajumbe wa chombo huru cha watumiaji maji kijijini  hapo.
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwasha  mashine ya kusukuma maji kwenye mradi wa maji kijiji cha Chididimo  manispaa ya dodoma muda mfupi baada ya kuzindua mradi huo.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi  (kushoto) akizungumza na  viongozi pamoja na  wananchi wa kijiji cha Chididimo kilichopo  manispaa ya Dodoma kuulinda na kuutunza mradi wa maji kijijini hapo muda mfupi mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuuzindua mradi huo leo.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi  (kulia) na katibu tawala Mkoa  Dodoma Ndg. Rehema Madenge wakifungua na kukinga maji kwenye mradi wa  maji kijiji cha Chididimo kilichopo manispaa ya Dodoma wakati wa uzinduzi wa mradi huo mapema leo hii. Wanaoshuhudia ni wananchi wa kijiji cha Chididimo.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi  akimtwika ndoo ya maji mdala Morleni Mwaluko mmoja wa wanakijiji cha chididimo,  maji hayo safi kwa  sasa yanapatikana kwa urahisi na kwa karibu  kijijini hapo baada ya kukamilika kwa  mradi wa maji wa kijiji hicho,
mkuu wa MKOA dodoma amezindua mradi huo mapema leo hii.
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi  (aliyeshika kibuyu katikati) akiimba na kuserebuka nyimbo za asili ya  kigogo pamoja na akinamama wa kijiji cha Chididimo manispaa ya Dodoma  kusherehekea muda mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua mradi wa  maji kijijini hapo leo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages