Kinachotarajiwa Kutoka Kwa JK Jioni Ya Leo... - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Kinachotarajiwa Kutoka Kwa JK Jioni Ya Leo...

Ndugu zangu,

Watanzania leo ni kama watu wenye kusubiri mtoto wa kwanza atakayezaliwa. Hakuna ajuaye kama ni wa kike au wa kiume.

Lakini , uhakika walio nao Watanzania ni kuwa kuna mtoto atakayezaliwa. Hapa ninamaanisha hotuba ya Rais ya leo itajikita katika suala la Katiba, ni kwa mwelekeo gani? Jibu lake haifahamiki na wengi wetu.

Bila shaka, kama Rais na Mkuu wa nchi, angependa kuwaona Watanzania wanabaki kuwa wamoja zaidi kama alivyorahisisha kwa Wazanzibar. Na kwamba naye atasisitiza umuhimu wa maoni ya wananchi kusikilizwa. Maana, ndio msingi wa Katiba na Utawala Bora.

Naam, pamoja na yote, Rais naye ni Mtanzania, na ana ndoto zake za Tanzania aitakayo baada ya yeye kuondoka. Aliwahidi Watanzania kuwa angetatua suala la Zanzibar ndani ya kipindi chake. Na sehemu ya kwanza ya kazi hiyo ameshaifanya. JK ndiye aliyerahisisha kupatikana kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. 

Miaka kumi iliyopita hakuna aliyedhani kuwa CUF na CCM wangeongoza kwa pamoja Zanzibar, kama ilivyo leo. Tofauti na waliomtangulia, JK ni Rais asiyetabirika na ndio maana hotuba yake ya leo imeleta hamu na shauku kubwa kwa Watanzania kutaka kuisikiliza.

Yumkini yaweza kuwa ' Mama' wa hotuba zote za JK. Kwamba ndiyo itakayoashiria moja ya mambo makubwa atakayoyaacha nyuma yake. Inahusu legacy.

Huu ni mtazamo wangu...

Maggid Mjengwa,
Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages