JUST IN: OBITUARY MKUU WA MKOA WA MARA MHE JOHN TUPA AFARIKI DUNIA WILAYANI TARIME LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JUST IN: OBITUARY MKUU WA MKOA WA MARA MHE JOHN TUPA AFARIKI DUNIA WILAYANI TARIME LEO



Mkuu wa mkoa wa Mara Mhe. John Gabriel Tupa 

(pichani, enzi za uhai wake) amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Tarime.  

Habari zilizothibitishwa zinasema Marehemu Tupa alianguka na kupoteza fahamu akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. John Henjewele,  alikokuwa akipokea taarifa kabla ya kufunga mafunzo ya mgambo wilayani humo.


Mara baada ya kuanguka juhudi za haraka zilifanyika za kumkimbiza hospitali ya Wilaya ya Tarime ambako alitangazwa kuwa ameshafariki mara alipofikishwa hapo.

Mwili wa Marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Mara ili kuhifadhiwa wakati taratibu za m,aziko zikiandaliwa.

Tutaendelea kuwapasha kinachoendelea kwa kadri taarifa zitavyokuwa zikitufikia

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages