Na Andrew Chale
KAMPUNI ya uuzaji wa bidhaa za majumbani na ofisini ya Home Shopping Centre (HSC) imemzawadia mshindi wake wa kwanza wa ‘pendezesha nyumba na HSC’, Rehane Jaffer zawadi ya sh 500,000. Shindano hilo linaendeshwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kwa jina la
‘Give a Way’. Mshindi alikabidhiwa hundi ya kiasi hicho cha pesa jijini
‘Give a Way’. Mshindi alikabidhiwa hundi ya kiasi hicho cha pesa jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Meneja Mauzo na Masoko wa HSC,
Nadhir Mubarak Bahayan ambaye aliwataka watanzania kushiriki
shindano hilo ambalo kila Ijumaa watakuwa wakijishindia sh. 500,000.
Nadhir Mubarak Bahayan ambaye aliwataka watanzania kushiriki
shindano hilo ambalo kila Ijumaa watakuwa wakijishindia sh. 500,000.
“Wateja wetu wa HSC, wanatakiwa kujiunga kwenye mtandao wetu wa facebook na kisha kututumia picha walizopamba ndani ya nyumba zao zitokanazo na bidhaa zetu,” alisema Nadhir.
Alisema shindano hilo litaendeshwa kwa mwezi mzima wa Machi 2014 .Mshindi huyo aliipongeza HSC kwa shindano hio na kusema ni faraja kwake na familia yake.
Aidha zoezi hilo ambalo litaendeshwa kwa muda wa mwezi mzima wa Machi huku kila Ijumaa ikitarajiwa kutangaza washindi na kukabidhiwa hundi siku inayofuata.

Nadhir aliwataka wateja wao kuwa na tabia ya kutembea kwenye
mtandao wa HSC, na kushiriki kupitia https://www.facebook.com/hsctz
mtandao wa HSC, na kushiriki kupitia https://www.facebook.com/hsctz

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)