HATUKUITISHA MKUTANO KUMNYOSHEA MTU KIDOLE - UINGEREZA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

HATUKUITISHA MKUTANO KUMNYOSHEA MTU KIDOLE - UINGEREZA

Na Mwandishi Maalum 

 Uingereza imeeleza kuwa , mkutano wa kimataifa uliofanyika mwezi uliopitia jijini London,  Uingereza na kujadili namna ya kukabiliana na biashara haramu ya wanyama pori duniani,  haukulenga kumnyoshea kidole mtu yeyote.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Uingereza katika Umoja wa  Mataifa, Balozi Peter Wilson wakati wa mkutano wa kundi la nchi marafiki kuhusu ujangili na biashara haramu ya wanyamapori.

Mkutano huo ulifanyika siku ya jumatano katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ujeruman katika  Umoja wa Mataifa, chini ya uenyekiti- weza wa Wawakilishi wa Kudumu wa Gabon na

Ujeruman. Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Balozi Tuvako Manongi alikuwa mmoja wa  washiriki wa kundi hilo la nchi marafiki. 
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kubadilisha mawazo miongoni mwa marafiki wa nchi hizo  ambazo zimefika 20. kuangalia ni kwa namna gani juhudi hizi za kukabiliana na ujangili na 

biashara haramu ya wanyama pori zinaweza kuungwa mkono ndani ya Umoja wa Mataifa  lengo likiwa ni kuzipa juhudi hizi msukumo wa kisiaza pamoja na ushiriki mpana zaidi.

Naibu Muwakilishi Balozi Wilson aliombwa kutoa muhtasari wa matokeo ya mkutano  huo wa kimataifa uliofanyika mwezi wa februari. Ambapo alianza kwa kusema, “ kwanza  ningependa kulieleza hili, mkutano ule hakuwa wakunyosheana vidole, tuliuitisha kwa  lengo la kujadiliana ni kwa namna gani tutashirikiana katika kuikabili biashara hii haramu ya

wanyamapori pamoja na ujangili”. 
Kwa ujumla Balozi Peter Wilson, aliwaambia wajumbe wa nchi hizo marafiki dhidi ya ujangili  na biashara haramu ya wanyamapori kwamba mkutano ulikuwa wa mafanikio makubwa kuliko  walivyokuwa wametarajia.

Akaeleza kuwa mwitikio wa ushiriki ulikuwa mkubwa sana, zaidi ya nchi 50 zilishiriki  wakiwamo marais watatu, akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na

Mashirika ya Kimataifa. 
Akasema kuwa mkutano huo ulitoka na tamko lenye nguvu ambalo linazungumzia mambo  mengi yakiwamo uimarishiji na uboreshaji wa sheria na sheria za makosa ya jinai, uwezeshwaji 

wa jamii zinazoishi katika maeneo ya wanyamapori kama sehemu ya kuwawezesha kuwa na maendeleo endelevu.

Akaongeza kuwa tamko hilo pia linazungumza udhibiti wa hitajio na soko la pembe za  tembo na raslimali nyingine zitokanazo na wanyamapori na akazitaka nchi nyingine ambazo

hazikuhushuria mkutano huo kuunga mkono tamko hilo. 
Akabainisha kwamba viongozi kutoka nchi za Afrika waliohudhuria mkutano huo, walionyesha  ushirikiano mkubwa na pia wao wenyewe walitoka na mpngo mkakati wao wa kukabiliana na  ujangili na biashara haramu ya wanayapori ikiwamo mikakati ya kuwalinda tembo

Naibu Muwakilishi huyo wa Uingereza pia ameeleza kwamba viongozi wakuu wa serikali  yake pamoja na Mwanamfalme wote wameonyesha utayari mkubwa katika kukabiliana na

changamoto hii. Aidha nchi kadhaa zikiwamo Marekani, Canada na Jumuiya ya Ulaya zimetoa ahadi za kuchangia raslimali fedha kusaidia juhudi hizo.

Wazungumzaji wengine katika mkutano huo walikuwa ni watendaji kutoka CITES, UNODC na UNEP ambapo katika ujumla wao, walieleza kwamba ili juhudi za kuukabili ujangili na  biashara haramu ya wanyapori ziweze kufanikiwa lazima pawepo juhudi na ushirikiano wa kimataifa.

Walieleza kwamba, ni kujidanganya kwamba nchi moja moja inaweza yenye peke yake  kukabiliana na hatimaye kuumaliza ujangili na biashara haramu ya wanyamapori kutokana na  ukweli kwamba, ujangili na biashara hiyo haramu mtandao wake ni mkubwa wenye sura ya uharifu wa kimataifa.

Baadhi ya wajumbe akiwamo Balozi Manongi, waliunga mkono umuhimu wa kundi hilo la  marafiki kutakafari mbinu na mikakati ya kupata uungwaji mkono wa kisiasa kutoka ndani ya  Umoja wa Mataifa. Na pia akasisitiza hoja ya udhibiti wa soko na hitajio la raslimali zitokanazo na wanyamapori.

Balozi Manongi akaeleza kwamba taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa zimeonyesha  utayari mkubwa wa kushiriki katika juhudi hizi za kuthibiti ujangili na biashara haramu ya  wanyamapori na kwamba itakuwa vema kwamba utashi na utayari huu kutoka kwa wadau mbalimbali ukaenziwa na wahusika wote.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages