balozi mdogo wa ethiopia amtembelea balozi mdogo wa tanzania dubai - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

balozi mdogo wa ethiopia amtembelea balozi mdogo wa tanzania dubai

 Balozi Mdogo wa Ethiopia Mhe. Yibeltal A. Alemu akikaribishwa na  Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dubai.
Balozi Mdogo wa Ethiopia Mhe. Yibeltal A. Alemu na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga katika mazungumzo. 

Katika mazungumzo yao wanadiplomasia hao  walipata fursa ya kuzungumzia njia muafaka na mbali mbali za kufanya kazi kwa karibu ili kuhakikisha wanavutia utalii na uwekezaji katika nchi zao hasa kwa kuwavutia wawekezaji kutoka wakubwa waliopo Dubai.

Mhe. Mjenga alimuomba Mhe. Yibeltal kubadilishana uzoefu wa Ethiopia katika kuvutia wawekezaji kutoka Dubai katika sekta ya kilimo. Alimuomba kuwa Maafisa wa Biashara kutoka Balozi zote mbili wakutane ili kubadilishana uzoefu huo ili Tanzania nayo iweze kuchukua mkondo huo kuwavutia wawejezaji kwenye kilimo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages