ARSENAL NJE LIGI YA MABINGWA, ATLETICO YAPETA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ARSENAL NJE LIGI YA MABINGWA, ATLETICO YAPETA

MUNICH, Ujerumani
Arsenal imeshindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Bayern Munich, kwenye Uwanja wa Allianz Arena jijini Munich, jana hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 3-1 kwa kuwa katika mechi ya kwanza Arsenal ilifungwa mabao 2-0.


Mfungaji wa Bayern alikuwa ni Bastian Schweinsteiger katika dakika ya 54, Arsenal ikasawazisha kupitia kwa Lukas Podolski katika dakika ya 57 kwa shuti kali baada ya nahodha wa Bayern, Philipp Lahm kujichanganya.
Mechi nyingine ya ligi hiyo ilishuhudia Atletico Madrid ikitoa kipigo cha mabao 4-1 kwa AC Milan, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-1, wafungaji wa Atletico wakiwa ni Diego Costa dakika ya tatu na 85, Arda Turan (40) na Raúl García (70), huku ikikumbukwa kuwa Milan ilichapwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza.

Bayern Munich: 1-Manuel Neuer; 21-Philipp Lahm, 4-Dante, 8-Javi Martinez, 27-David Alaba; 6-Thiago Alcantara, 31-Bastian Schweinsteiger; 10-Arjen Robben, 19-Mario Goetze, 7-Franck Ribery; 9-Mario Mandzukic
Substitutes: 22-Tom Starke, 5-Daniel van Buyten, 13-Rafinha, 17-Jerome Boateng, 25-Thomas Mueller, 39-Toni Kroos, 14-Claudio Pizarro
Arsenal: 21-Lukasz Fabianski; 3-Bacary Sagna, 4-Per Mertesacker, 6-Laurent Koscielny, 5-Thomas Vermaelen; 8-Mikel Arteta, 11-Mesut Ozil, 15-Alex Oxlaide-Chamberlain; 19-Santi Cazorla, 12-Olivier Giroud, 9-Lukas Podolski
Substitutes: 13-Emiliano Viviano; 25-Carl Jenkinson, 7-Tomas Rosicky, 20-Mathieu Flamini, 44-Serge Gnabry, 45-Isaac Hayden

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages