Mke wa Godfrey Mgimwa, Mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM Robi Mgimwa akimuombea kura mme wake katika mkutano wa kufunga kampeni kata ya Nzihi jimbo la Kalenga leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bw. Hassan Mtenga katikati ni Godfrey Mgimwa mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini na mtangazaji wa ITV Godwin Gondwe mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihani msiba katika kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi
Salim Asas Abri kamanda wa vijana CCM mkoa wa Iringa alikuwa ni mmoja wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
Umati wa wananchi waliofurika katika mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara na Waziri wa Fedha na Uchumi Mwigulu Nchemba akihutubia katika mkutano huo.
Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Bw. Akwilombe akihutubia katika mkutano huo
Mkurugenzi wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku katikati akiwa na wahadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini kulia ni Simon Berege na Godwin Gondwe kushoto.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifuatilia hotuba ya Mbunge wa jimbo la Mwibara Kangi Lugora hayupo pichani wakati alipokuwa akihutubia mkutano huo, kushito ni Mwigulu Nchemba Naibu Katibu Mkuu Bara na Godfrey Mgimwa mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM.
Mbunge wa Mwibara Kangi Lugora akihutubiwa wananchi katika mkutano huo.
Mbunge wa jimbo la Ludewa aDeo Filikunjombe kiwaomba wana Kalenga kumpa kura za ndiyo Godfrey Mgimwa.
Msanii Dokii akitumbuiza katika kutano huo uliofanyika leo kata ya Nzihi.
-





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)