zungu la unga ladakwa na kilo 5 za 'sembe' uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere dar es salaam - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

zungu la unga ladakwa na kilo 5 za 'sembe' uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere dar es salaam

Raia wa Henellic, Alexamdrios Atanasios, amekamatwa maafisa wa usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumapili usiku Februari 24, 2014, akiwa na kilo tano za madawa ya kulevya.

 Habari zinasema mzungu huyo alikamatwa wakati wa upekuzi, akijiandaa kupanda ndege ya Swiss air kueleke jijini  Zurich, Uswisi. 

Madawa hayo yalikutwa yakiwa yamefichwa kwenye “sakafu” ya begi lake baada ya mitambo ya kisasasa yaupekuzi, kugundua kuwa kulikuwa na ‘mzigo’.

Habari zinasema, kwa sasa mtuhumiwa anashikiliwa kwenye kituo cha polisi cha uwanjani hapo  akisubiri taratibu za kisheria ili afungukliwe mashtaka.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages