UONGOZI WA MLIMANI CITY MNALIONA HILI; ENEO ZIMA LA MAEGESHO YA MAGARI MLIMANI CITY INALINDWA NA MTU MMOJA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UONGOZI WA MLIMANI CITY MNALIONA HILI; ENEO ZIMA LA MAEGESHO YA MAGARI MLIMANI CITY INALINDWA NA MTU MMOJA

 Hii ni sehemu moja tu ya Mlimani City Mall ambayo kuna mlinzi mmoja tu eneo la kupaki magari hii ni hatari sana kwa wananchi wanaokuja na magari yao eneo hili maana hakuna ulinzi wa kutosha. Hivi kweli mtu huyu mmoja anaweza kulinda eneo lote la Mlimani City au kuna mchezo unachezwa.
 Sehemu hii pia haina mlinzi anayelinda magari yanayopaki Mlimani City  Mall hii ni hatari kwa watu wenye magari yao maana wezi ni wengi eneo hili kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi mzuri. Unaweza kujiuliza hivi kweli hakuna walinzi wa kutosha wa kukaa kwenye sehemu hii maana kwa siku magari yanayoingia na kutoka Mlimani City ni zaidi ya 400.
Hivi kweli uongozi wa Mlimani City Mall unafanya hata ukaguzi eneo hili kuona kama kuna tatizo, mpaka blog yetu hii ilipopita hapo na kuliona hili tatizo kwa wakati mdogo. Ukitizama katika picha hiyo ya hapo juu unaona hakuna walinzi sehemu hizo mbili . Hivi kweli wizi ukitokea eneo hili nani atarahumiwa kati ya uongozi na walinzi wa Mlimani City.
Huu ndio mwenekano halisi wa magari yakiwa yamepaki na kuna mlinzi mmoja kwa juu ambaye hawezi kuona magari yote kwa kupitia juu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages