UKUMBI WA KISASA KABISA WA BNN CONVENTION CENTER WAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM MWISHONI MWA WIKI. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UKUMBI WA KISASA KABISA WA BNN CONVENTION CENTER WAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM MWISHONI MWA WIKI.

Mwenyekiti wa Makampuni ya BNN Mh Paul Koyi akimkaribisha Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdallah Kigoda katika uzinduzi wa Ukumbi na Lounge Mpya na Ya Kisasa kabisa ya BNN iliyopo katika Jengo la Quality Center barabara ya Nyerere Mwishoni Mwa Wiki.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Dkt Abdallah Kigoda (Katikati) akikata utepe kuashiria kuwa Ukumbi wa BNN pamoja na lounge ya BNN vimezinduliwa rasmi katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Jengo la Quality center, Kushoto ni Mwenyekiti wa Makampuni ya BNN Mh Paul Koyi na Wa Kwanza kulia ni Grace Koyi akifuatiwa na Mwakilishi wa Chivas Nchini Tanzania Bw Adam Kawa.
Mwenyekiti wa Makampuni ya BNN Mh Paul Koyi ambao ni wamiliki wa Ukumbi na Lounge Mpya kabisa ya BNN uliopo katika Jengo la Quality center akiwakaribisha Wageni waalikwa pamoja na Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Ukumbi mpya na wa kisasa wa BNN pamoja na BNN Lounge mwishoni mwa wiki
Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Ukumbi na Lounge Mpya na ya Kisasa na ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdallah Kigoda akitoa maneno ya shukrani na pongezi kwa uongozi mzima wa BNN kwa kuamua kuwekeza, Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi huo wa BNN uliopo katika Jengo la Quality Center.
Mwakilishi wa Jameson Tanzania Bw Adama Kawa (Kulia) akimkabidhi mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Dkt Abdallah Kigoda (kushoto) boksi la Kinywaji cha Jameson. Katikati ni Mwenyekiti wa Makampuni ya BNN Mh Paul Koyi.
Mwenyekiti wa Makampuni ya BNN Mh Paul Koyi (mwenye miwani) Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mh Dkt Abdallah Kigoda katika lounge ya BNN iliyopo katika Jengo la Quality Center wakati wa uzinduzi wa Ukumbi pamoja na Lounge ya BNN uliofanyika Mwishoni mwa Wiki.
Mwenyekiti wa Makampuni ya BNN Mh Paul Koyi akimkaribisha ndani ya BNN lounge Mgeni rasmi Mh Dkt Abdallah Kigoda wakati wa uzinduzi wa Ukumbi na lounge ya BNN uliofanyika Mwishoni mwa wiki katika Jengo la Quality Center Barabara ya Nyerere.
Mgeni rasmi Dkt Abdallah Kigoda akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Ukumbi na Lounge Mpya kabisa na ya kisasa iliyopo katika Jengo la Quality Center.
Mwakilishi wa Jameson Tanzania Bw Adam Kawa (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa katika uzinduzi wa Ukumbi Mpya wa BNN uliopo katika Jengo la Quality Center.
Mwakilishi wa Chivas Nchini Tanzania Bw Adam Kawa kaibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa katika Uzinduzi wa Ukumbi wa BNN uliofanyika mwishoni mwa Wiki.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Ukumbi Mpya na Lounge Mpya ya BNN uliopo katika Jengo la Quality Center Mwishoni mwa Wiki.
Mdau Julius Koyi akijiachia mbele ya Kamera ya Lukaza Blog wakati wa uzinduzi wa Ukumbi mpya na wa kisasa wa BNN uliopo katika Jengo la Quality Center.

 Jumamosi ya Mwisho wa Wiki kulifanyika hafla ya uzinduzi wa kituo cha mikutano cha BNN Convention Centre, kilichopo ndani ya jengo la Quality Centre, Barabara ya Nyerere, jijini Dar es salaam, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dr. Abdallah Kigoda (Mbunge).

Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Kampuni ya Pernord Ricard Sub-Saharan Africa, watoaji wa pombe za Chivas, Ricard, Malibu, Jameson, The Glenlivet, Absolut Vodka, Ballantines, Kahlua, Havana Club, Beefeater, Martell, Royal Salute na Perriel Jolet.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages