AJALI MBAYA YATOKEA MWEKA, MOSHI YAHUSISHA DALADALA NA LAND CRUISER - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AJALI MBAYA YATOKEA MWEKA, MOSHI YAHUSISHA DALADALA NA LAND CRUISER

Ajali imehusisha gari ya abiria aina ya hiace inayofanya safari zake kati ya Mweka na moshi mjini  na landcruiser VX iliyokuwa  imewabeba  wanafunzi wa chuo cha usimamizi na uhifadhi wa wanyama pori Mweka kilichopo Mweka , Moshi vijijini.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo bwana Fred Mushi amesema kuwa gari aina ya landcruiser VX iligonga daladala  hiyo iliyo kuwa imesimama kupakia abiria kwenye kituo kimoja maarufu kwa jina la Kona. Ajali hiyo imetokea muda wa saa 10.30 jioni hii
Gari aina ya landcruiser VX iliyokuwa na wanafunzi toka chuo cha Mweka
ikiwa imezama kwenye mtaro  na kuharibika vibaya baada ya ajali hiyo mbaya iliyotokea jioni hii
mashuhuda walikokuwa eneo la tukio wakilitazama gari aina ya landcuriser iliyokuwa imezama kwenye mtaro baada ya ajali hiyo iliyotokea jioni hii na kusababisha majeruhi
daladala iliyogongwa vibaya na landcuriser ikiwa imeharibika vibaya ubavuni kiasi cha kutoweza kutembea tena lakini Taarifa za awali hali ya dereva wake   inasemekana kuwa mbaya pia idadi ya majeruhi mpaka
tunaenda mitamboni  haijajulikana.tutaendelea kukujuza jinsi taarifa zitakavyofikia kuhusu hali na idadi Ya majeruhi.PICHA NA HABARI NA mdau WITO MSAFIRI 


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages