Taarifa ya CHADEMA Kuhusu Kikao cha Kamati Kuu Leo hii hapa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taarifa ya CHADEMA Kuhusu Kikao cha Kamati Kuu Leo hii hapa

 John Mnyika-Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema
--
   CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO.

Kutokana na maswali kutoka kwa wanahabari wa vyumba mbalimbali vya habari juu ya agenda za kikao cha Kamati Kuu kesho,Chama kimetoa kauli ifuatayo;

Ni kweli kutakuwa na mkutano maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni tatu;

Mosi: Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya
kupitishwa kwa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa 2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.



Pili: Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao.

Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na wamewasilisha utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.

Tatu: Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014

Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.

John Mnyika
Mkurugenzi wa Mawasiliano

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages