MASHABIKI wa Michael Schumacher leo walimtumia salamu za kuadhimisha kutimiza mwaka wa 45 tangu kuzaliwa kwake wakati akiwa amelazwa hospitalini kutokana na kujeruhiwa vibaya kichwani wakati alipokuwa akishiriki mchezo wa kuteleza kwenye barafu maeneo ya Alps nchini Ufaransa.
Schumacher ambaye ni mshindi wa mara kadhaa wa mbio za kuendesha magari za Formula One (F1) hivi sasa anapata matibabu akiwa hajitambui baada ya kufanyiwa operesheni ya kichwa ambapo alikipigiza kwa bahati mbaya kwenye jiwe.
Schumacher ambaye mashabiki wake humwita Schumi, ndiye dereva mwenye mafanikio zaidi katika mashindano ya F1 akiwa ameshinda mara 91 kabla ya kustaafu mwaka 2012.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)