USAID YAAHIDI KUENDELEA KUISAIDIA TFDA KATIKA UDHIBITI WA USALAMA NA UBORA WA BIDHAA ZA CHAKULA, DAWA, VIPODOZI NA VIFAA TIBA TANZANIA. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

USAID YAAHIDI KUENDELEA KUISAIDIA TFDA KATIKA UDHIBITI WA USALAMA NA UBORA WA BIDHAA ZA CHAKULA, DAWA, VIPODOZI NA VIFAA TIBA TANZANIA.

Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo akikabidhi tozo maalum kwa Mkurugenzi wa USAID Bi. Sharon L. Cromer katika hafla iliyofanyika TFDA makao Makuu.
Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya TFDA na ujumbe wa USAID wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo akiuonesha ujumbe wa USAID moja ya vitabu rejea vya viwango vinavyotumika katika maabara ya TFDA.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Sharon L. Cromer ameahidi kuendelea kushirikiana na TFDA katika kuhakikisha afya ya wananchi inalindwa kwa kuisaidia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika kuijengea uwezo kwenye masuala ya udhibiti wa usalama na ubora wa bidhaa za
chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba nchini. 

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17/12/2013 katika ziara ya ujumbe wa USAID iliyofanyika Makao Makuu ya TFDA kwa lengo la kujionea ufanisi wa utendaji wa Mamlaka kufuatia misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa na Shirika hilo la kimaendeleo kwa TFDA kuanzia mwaka
2011 hadi sasa.

USAID imekuwa ikiisaidia TFDA katika kuwajengea uwezo watumishi wake hususan udhamini wa mafunzo kwa wakaguzi wa dawa, mafunzo kwa watumishi kuhusu mifumo bora ya utendaji kazi na utoaji huduma pamoja na manunuzi ya vifaa vya maabara ya Mikrobiolojia kwa lengo la kuendelea
kukidhi vigezo vya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo, alikabidhi tuzo maalum kwa shirika la USAID ikiwa ni alama ya kutambua mchango wa USAID katika mafanikio yaliyofikiwa na Mamlaka kwa kipindi cha miaka 10 (2003-2013)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages