Serikali ya Tanzania na Shirikisho la Ujerumani zimesaini makubaliano ya msada wa Fedha za Ulaya EURO Milioni 55.5 sawa na Shilingi Bilioni 121.89 za Kitanzania kusaidia sekta ya Maji, Umeme na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Serikali ya Tanzania na Shirikisho la Ujerumani zimesaini makubaliano ya msada wa Fedha za Ulaya EURO Milioni 55.5 sawa na Shilingi Bilioni 121.89 za Kitanzania kusaidia sekta ya Maji, Umeme na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile akibadilishana mikataba ya makubaliano na Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam.
 Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikataba iliyosainiwa kati ya Serikali yake na Serikali ya Tazania. Kushoto ni Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam Wolfgang Solzbacher.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile akizungumza na waandishi wa habari9hawapo pichani) baada ya kusaini mikataba ya makubaliano na Serikali ya Ujerumani.Katikati ni Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumzia jinsi mikataba hiyo itakavyonufaisha Hifadhi ya Serengeti huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam Wolfgang Solzbacher na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel, wakimsikiliza.
Picha ya pamoja kutoka kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel, atibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile(mwenye suti ya kaki), Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam Wolfgang Solzbacher (mwenye tai nyekundu), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Modestus Lilungulu na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi.Picha na Hussein Makame, MAELEZO
----
 Hussein Makame, MAELEZO
SERIKALI ya Tanzania na ile ya Shirikisho la Ujerumani zimesaini makubaliano ya msada wa Fedha za Ulaya EURO Milioni 55.5 sawa na Shilingi Bilioni 121.89 za Kitanzania kusaidia sekta ya Maji, Umeme na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Akizungumza baada ya utiaji saini huo uliofanyika Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile alisema katika makubalianao ya kwanza Serikali ya Ujerumani itatoa EURO Milioni 20.5 sawa na Shilingi Bilioni 45.059.

Alisema fedha hizo zitatumika kusaidia Kuhifadhi wa Hifadhi ya Serengeti katika Kuendeleza na Kutunza maliasili ya hifadhi hiyo, kuboresha miundombinu ya kijamii na kujenga barabara katika wilaya za Loliondo na Srengeti.

 “Mkataba wa makubaliano wa pili utawezesha Serikali ya Ujerumani kutoa mchango wa EURO Miloni  20 sawa na Shilingi Bilioni 43.96 kusaidia kusambaza umeme Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania “ alisema Dk. Likwelile.

Alisema msaada huo utasaidia kuunganisha wananchi wa vijijini 32,500 katika maeneo hayo kupata umeme na kuunganisha Gridi ya Taifa hadi kwenye Mtambo wa Kuzalisha Umeme wa maji wa Rusumo na kuuza umeme nchini Rwanda na Burundi.

Dk. Likwelile aliongeza kuwa mkataba wa makubaliano wa tatu utaiwezesha Serikali ya Ujerumani kutoa msaada wa EURO Milioni 15 sawa na Shilingi Bilioni 32.97 kusaidia Sekta ya Maji kupitia Programu ya Maendeleo awamu ya pili.

Alifafanua kuwa kupitia programu hiyo msaada huo utafabikisha utekelezaji wa Usimamizi wa Rasilimali ya Maji, Usambazaji wa maji Vijijini na Mijini na Kuimarisha Taasisi na Kujengea Uwezo Sekta ya Maji.

Aliihakikishia Serikali ya Ujerumani kuwa fedha hizo zitatumika vizuri na kuwanufaisha wananchi wa maeneo husika na aliwaomba wanachi husika wathamini msaada huo kwa kutunze miradi ya maendeleo katika maeneo hayo.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel msaada huo unathibitisha kuwa Serikali yake imedhamiria kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo ili kuchangia kuboresha ustawi na utajiri wa wananchi wa Tanzania.  

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Modestus Lilungulu alisema msaada huo utasaidia kutekeleza Mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa ambao lengo lake ni kufikisha huduma ya maji vijijini kwa asilimia 74 na mijini asilimia 90 ifikapo mwaka 2015.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi alisema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muwafaka kutokana na changamoto ya ongezeko la idaidi ya watu lililosababisha kuongezeka kwa huduma kwa binadamu kuongezeka.

Kwa zaidi ya miongo mitano iliyopita Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Ujerumani umefanikisha misaada yenye thamani ya Fedha za Ulaya EURO Bilioni 2.03 huku Serikali ya Ujerumani ikisaidia sekta za Umeme, maji, mazingira na Afya.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages