Rais Jakaya Kikwete Aelekea Nchini Marekani kufanyiwa Uchunguzi wa Afya Yake. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Rais Jakaya Kikwete Aelekea Nchini Marekani kufanyiwa Uchunguzi wa Afya Yake.

 Rais Jakaya Kikwete
----
 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA  
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya jana, Jumatano, Desemba 18, 2013, kwenda Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za uchunguzi wa afya yake na kwa kutilia maanani siku za kusafiri kwenda Marekani na kurudi nchini, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nchini Alhamisi ya wiki ijayo, Desemba 26, 2013.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Desemba, 2013

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages