Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi ameungana na Wawakilishi wa Mataifa mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa, katika kusaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Kwanza wa Afrika ya Kusini Huru, Mzee Nelson Mandela.
Kitabu hicho kimefunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini katika Umoja wa Mataifa. Katika Salamu zake, Balozi Tuvako Manongi ameandika " kwa niaba ya Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, ninawasilisha salamu zetu za rambirambi kwa serikali, wananchi, familia na wapendwa wa Marehemu Mhe. Mzee Nelson Mandela.
Tunaungana nanyi katika kuombeleza msiba wa kiongozi huyo ambaye alijitolea katika kuikomboa Afrika ya Kusini. Mchango wake katika kuwaunganisha wana wa afrika ya kusini licha ya tofauti zao za kikabila ni jambo lililoihamasisha dunia yote. Sisi katika Tanzania tunajivunia sana kumfahamu Madiba".
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)