Kikundi cha
Nahodha Benedicto Chamba kutoka Mara wakishangilia na Kikombe mara baada ya
kutwaa ubingwa wa mashindano ya mbio za mitumbwi upande wa Wanaume, zilizofanyika
jana katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza kwa udhamini wa bia ya Balimi Extra
Lager.Wa pili kulia ni Meya wa Manispaa ya jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula na
Meneja mauzo na Usambazaji waTBL, Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki.
Kikundi cha
Nahodha Benedicto Chamba kutoka Mara wakishangilia na Kikombe mara baada ya
kutwaa ubingwa wa mashindano ya mbio za mitumbwi upande wa Wanaume, zilizofanyika
jana katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza kwa udhamini wa bia ya Balimi Extra
Lager.Wa pili kulia ni Meya wa Manispaa ya jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula na
Meneja mauzo na Usambazaji waTBL, Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki.
Nahodha
Regina Kazungu kutoka jijini Mwanza akishangilia na Kikombe mara baada ya
kuibuka mabingwa upande wa Wanawake wakati wa mashindano yam bio za mitumbwi
Kanda ya Ziwa yaliyofanyika jana katika ufukwe wa Mwaloni Mwanza kwa udhamini
wa bia ya Balimi Extra Lager.Kushoto ni Meya wa Manispaa ya jiji la Mwanza,
Stanslaus Mabula.
Picha ya
pamoja ya kikundi cha nahodha Regina Kazungu kutoka jijini Mwanza wakiwa na
kikombe mara baada ya kutwaa ubingwa wa mbio za mitumbwi upande wa wWanawake
zinazodhaminiwa na bia ya Balimi Extra Lager Kanda ya ziwa.
Na Mwandishi
Wetu, Mwanza
KIKUNDI wapiga
kasia Wanaume kinachoongozwa na nahodha Benedicto Chamba kutoka Mkoa wa Mara kimetwaa
ubingwa wa Kanda ya Ziwa wa mashindano ya mbio za Mitumbwi zinazodhaminiwa na Kampuni
ya Bia nchini kupitia Bia ya Balimi Extra Lager na hivyo kujitwalia zawadi ya
fedha taslimu Shilingi 2700,000/=,Kikombe pamoja na medali za dhahabu.
Nafasi ya
pili ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Eliud Prosper kutoka Gagera ambao
walizawadiwa fedha taslimu shilingi 230,000/=,nafasi ya tatu ilichukuliwa na
kikundi cha nahodha Toto Benedicto kutoka Ukerewe ambao walizawadiwa fedha
taslimu shilingi 1700,000/=,nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha nahodha
JJ. Buda kutoka Mara ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 900,000/=na
nafasi ya tano hadi kumi walipewa kufuta jasho cha silingi 400,000/= kila
kikuni ambao ni kikundi cha nahodha Totoji Mazige kutoka Ukerewe,kikundi cha
Constantine Lusalago kutoka Mwanza, kikundi cha Bernard Charles kutoka
Mara,kikundi cha Lenard Zungu Mwanza,kikundi cha Daniel Mugenda Mwanza na
kikundi chaSimon Fundi kutoka Ukerewe.
Upande wa
Wanawake kikundi cha nahodha Regina Kazungu kutoka Jijini Mwanza walitwaa
Ubingwa wa Kanda ya Ziwawa mashindano
hayo na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 2300,000/=,kiombe pamoja na
medali za dhahabu.
Nafasi ya
pili ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Nyamizi Deo kutoka Musoma ambao
walizawadiwa fedha taslimu shilingi 1700,000/=,nafasi ya tatu ilichukuliwa na
kikundi cha nahodha Jenifaer Elias kutoka Ukerewe,nafasi ya nne ilikwenda kwa
kikundi cha nahodha Muhate Mwocha kutoka Ukerewe na nafasi na tano hadi kumi
walizawadiwa kifuta jasho cha fedha taslimu shilingi 250,000/=
Meneja mauzo
na usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa, Maalaki Sitaki aliwapongeza washiriki wote
tangu mashindano hayo yalipoanza kwangazi ya mikoa hadi Kanda yamekuwa ya amani
nautulivu lakini pia aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2013 na kuwaomba wakautumie
vizuri ubingwa wao kwa maandailizi ya mashindao hayo mwakani na wakawe mabalozi
wazuri wa bia ya Balimi Extra Lager.
Nae mgeni
rasmi, Meya wa manispaa ya jiji la Mwanza kwa niaba ya Mkoa Inginia Evaristo
Ndikilo, Stanslaus Mabula, aliipongeza TBL, kupitia bia yake ya Balimi Extra
Lager kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo kwani kupia mashindano hayo ni
mchango mkubwa sana kwa jamii na kwa Serikali inalitambua hilo na iko pamoja na
TBL kusaidia pale itakapo hitaji msaada.
Mwisho
mabula aliwapongeza mabingwa wote na kuwatakia kusherekea ubingwa wao kwa amani
na pia aliwataka wakawe mabalozi wazuri wa bia ya balimi extra lager ili
wadhamini waendelee kudhamini mashindano hayo.
Fainali za
mashindano yam bio za mitumbwi zilihusisha Mkoa wa Kigoma, Kagera, Mwanza ,Mara
na Kisiwa cha Ukerewe ambacho pia hubeba hadhi ya Mkoa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)