MAN UNITED, MAN CITY ZAKWEPANA NUSU FAINALI YA KOMBE LA LIGI….SPURS MAJANGA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAN UNITED, MAN CITY ZAKWEPANA NUSU FAINALI YA KOMBE LA LIGI….SPURS MAJANGA

Head boy: Modibo Maiga scores the goal which booked West Ham's place in the final four following their 2-1 win at Spurs
Kijana akipiga ndosi: Modibo Maiga akifunga bao lililoipa tiketi ya kucheza nusu fainali klabu ya West Ham kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Spurs

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
MANCHESTER united atavaana na Sunderland katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la ligi wakati Manchester City itapambana na wagonga nyundo wa London, West Ham.
David Moyes alitinga hatua hiyo baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stoke City jana usiku, mabao yakifungwa na Ashley Young dakika ya 61  pamoja na beki wa kushoto Patrice Evra dakika ya 78 .
Sunderland waliifunga Chelsea mabao 2-1 siku ya jumanne, huku  Ki Sung-Yueng akifunga bao la ushindi dakika za mwisho za muda wa nyongeza.
Katika mchezo mwingine, mshambuliaji Emmanuel Adebayor alirejea uwanjani na kufunga bao moja wakati timu yake, Tottenham Hotspur ikifungwa 2-1 na West Ham United, mabao ya Jarvis dakika ya 80 na Maiga dakika ya 85.

Man United sasa itamenyana na Sunderland katika Nusu Fainali ya michuano hiyo maarufu kama Capital One, wakati West Ham itakipiga na Manchester City.
Screamer: Tom Cleverley celebrates Ashley Young's stunning opener in Manchester United's quarter-final win at Stoke Tom Cleverley akishangilia bao la kwanza la Ashley Young wakati Manchester akisaka tiketi ya kucheza nusu fainali ya kombe la Ligi dhidi ya Stoke
City slickers: Man City celebrate Edin Dzeko's second goal during their 3-1 win at Leicester CityKatika mchezo mwingine, Man City waliichapa Leicester City mabao 3-1. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages