KINANA AHITMISHA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA KWA KISHINDO JIONI YA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

KINANA AHITMISHA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA KWA KISHINDO JIONI YA LEO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wakazi wa Mbeya mjini, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni hii katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.
 Katibu NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wananchi wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.

 Sehemu ya Wakazi wa jiji la Mbeya Mjini wakishangilia jambo wakati Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye alipokuwa akihutubia,katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yao katika mkoa huo.
 Pichani kati ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakiwapungia mikono wakazi wa jiji la Mbeya waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika katika uwanja wa Rwanda Nzovwe,nyuma ni Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa Dkt.Asharose Migiro.
  Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye Bajaj huku akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi na Wanachama wa CCM,waliokuwa wamejipanga barabarani kushuhudia tukio hilo la aina yake wakati Ndugu Kinana akiwa ameambatana na msululu wa Bajaji akielekea kwenye mkutano wa hadhara,anaekimbia pichani kulia ni Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
 Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi na Wanachama wa CCM,waliokuwa wamejipanga barabarani kushuhudia tukio hilo la aina yake wakati Ndugu Kinana akiwa ameambatana na msululu wa Bajaji akielekea kwenye mkutano wa hadhara.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages