Aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akipozi mara baada ya kulamba Nondozzz ya shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine jijini Mwanza.
Hoyce Temu akipata Ukodak na Mdau wa tasnia ya habari nchini.
Hoyce Temu katika pozi na marafiki zake mara baada ya kulamba Nondozz.
Pongezi pia ziende kwa Dada Lulu Musa Afisa Uhusiano wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kwa kulamba Nondozz ya shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya Umma katika chuo cha St. Augustine University kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa Juma.
Mbali na kula Nondozz kwenye siku hiyo maalum Hoyce Temu ambaye pia ni Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania aliamua kufanya mahojiano na baadhi ya wahitimu kwa ajili ya kipindi chake.
Mlimbwende Hoyce Temu akizungumza na mwandishi wa habari wa ITV kuhusiana na taalum aliyoipata itakavyoweza kuboresha utendaji wake kazini pamoja na kuendelea kuisaidia jamii inayomzunguka kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania.
Mwanandishi wa habari wa kituo cha ITV Shaban Tole akimpongeza Hoyce Temu.
Hoyce Temu katika picha ya kumbukumbu na marafiki.
Hoyce Temu akiondoka eneo la tukio na furaha isiyo na kifani.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)