Action
Music Tanzania (AMTZ) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na
mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza desemba 19 mwaka huu, lengo
likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho
kwa weledi na utaalamu zaidi.
Mafunzo
yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita,
kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za
asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya
mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.
Mafunzo
hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge karibu
na magorofa ya jeshi ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao
kwa simu namba 0686928828 au barua pepe, actionmusictz@yahoo.com, Like Facebook Page au tembelea www.amtz.org
Mwalimu Abeid Mussa akitoa maelekezo ya wakati wa mazoezi ya kufanya onyesho la muziki
Mwalimu wa Kinanda Prosper Shirima (katikati) akifundisha
Mwalimu wa Gita, Ashimba (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kupiga chombo hicho
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)