Mkuu wa Kitengo cha Affluent Banking wa benki ya Barclays Tanzania Ms Neema Rwehumbiza akiongea na waandishi wa habari waliofika katika ofisi za Benki hiyo katika tawi lililopo Alpha House barabara ya Ali hassan Mwinyi kwaajili ya kushuhudia washindi wa Droo ya Pili ya "Double your Saving"kutoka benki ya Barclays.
Mmoja wa Wafanyakazi wa Benki ya Barclays tawi la Alpha house Barabara ya Ali Hassan Mwinyi akizungusha pipa lenye kuponi za washiriki wa droo ya pili ya "Double Your Saving" kwaajili ya kupata washindi wa tano wa Mwezi November, huku akiongozwa na afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Mkuu wa Kitengo cha Affluent Banking wa benki ya Barclays Tanzania Ms Neema Rwehumbiza akisoma jina la Mshindi wa Kwanza aliyepatikana mara baada ya pipa hilo kuzungushwa katika droo ya pili ya "Double your saving' kutoka Benki ya Barclays Tanzania iliyochezeshwa leo katika Ofisi ya Benki hiyo katika tawi lililopo barabara ya Ali Hassani Mwinyi
Mmoja wa Wafanyakazi wa Benki ya Barclays tawi la Alpha house Barabara ya Ali Hassan Mwinyi akichukua moja ya kuponi za washiriki wa droo ya pili ya "Double your Saving" kwaajili ya kumtaja mshindi wa Pili katika droo iliyochezeshwa leo na Kupelekea kupatikana kwa washindi watano ambao kila Mmoja ataondoka na Kitita Cha shilingi Milioni Moja
.................................
5 Disemba 2013 , Baclays Bank Tanzania leo imefanya droo yake ya Pili kwa wateja wake katika kampeni ijulikanayo kama "Double Your Saving". Kampeni hii ilianza rasmi tarehe 16 septemba 2013 na itaendelea hadi tarehe 16 Januari 2014.
Kila Mwezi, droo hii itawapatia wateja watano nafasi ya kujishindia hadi shilingi milioni moja za kitanzania kila mmoja kwa kipindi chote cha kampeni. Droo za mwezi, zitakuwa zinafanyika wiki ya mwisho ya mwezi husika.
Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo Cha Affluent cha Benki ya Baclays Ms Neema Rwehumbiza amesema; "Ushiriki upo wazi kwa wateja wote binafsi(waliopo na wapya) kupitia akaunti zao za akiba na za hundi.
Wanachotakiw kufanya ni kuongeza na kutunza akiba zao kwa kiwango cha Shilingi laki tatu (300,000) za kitanzania au zaidi. Kiwango hiko kitampa mteja nafasi ya kushiriki katika droo ya mwezo husika tu. Baada ya kuongeza akiba kwa kiwango husika, mteja ataingia kwenye droo ya mwezi na kupata nafasi ya kujishindia hadi shilingi milioni moja za Kitanzania. Kila ongezeko la shilingi laki tatu litampatia mteja nafasi moja ya kushiriki.
Wateja wote watakaoongeza salio kwenye akaunti zao kwa shilingi laki tatu au zaidi katika kipindi hiki cha kampeni wanajipatia nafasi ya kushinda zawadi kubwa kabisa ya shilingi za kitanzania Milioni Thelathini (30,000,000) mwishoni mwa kampeni hii.
Aliongeza kuwa, "hii ni droo ya pili ambao tunapata washindi wengone watano. Baclays inawapongeza washindi wote na kuhamasisha watanzania wote kushiriki katika kampeni hii hususani katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa Mwaka.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)