WEMA SEPETU AFUNGUKA KUHUSU MASTAR WALIOGOMEA MSIBA WA BABA YAKE. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WEMA SEPETU AFUNGUKA KUHUSU MASTAR WALIOGOMEA MSIBA WA BABA YAKE.



Wema Sepetu 
Kupitia kipindi chake cha ‘In My Shoes’ cha jana, Wema Sepetu alieleza jinsi alivyojisikia baada ya baadhi ya waigizaji wenzie wa club ya Bongo movie kugoma kuhudhuria msiba wa baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, mwishoni mwa mwezi uliopita kwa madai kuwa yeye hakuwa akifanya hivyo kwenye misiba mingine. .......

“Imeshatokea, wameacha kuja kwenye msiba, ni wao,” alisema Wema. Sio Bongo movie nzima, ni baadhi tu ya watu ambao wanauelewa na upeo mdogo ambao waliamua kutokuja. Lakini niliona Bongo movie wengi, walikuwepo marafiki zangu wengi, akina Batulli, akina Esha, Wolper alikuja, Lulu, JB alikuja, Jokate alikuja, Adam Kuambiana alikuja. Ambaye napenda nimpe my special thanks and appreciation, ambaye alijitolea from the beginning wa msiba mpaka to the end ni Dokta Cheni kwakweli. Dr Cheni, I thank you na ntazidi kumshukuru,” alisema. 

“Marafiki zangu kama akina Kajala, akina Zamaradi, wale sio marafiki, wale tayari ni ndugu, kwahiyo siwezi kuwaweka kwenye appreciation wala kwenye thanks.” 

Katika kipindi hicho pia, Wema alisema yeye na ndugu zake walijua kuwa baba yako ni muumini wa dhehebu la Roman Catholic siku chache kabla ya kufariki dunia.

Special "In My Shoes" Episode dedicated to the late Daddy Sepetu itakuwa kwa blog soon. Stay tuned

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages