WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU, MAANA UFALME WA MBINGU NI WAO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU, MAANA UFALME WA MBINGU NI WAO

Kuna wakati papa akiwa amesimama anazungumza mtoto huyo alimkumbatia miguu lakini papa alimwacha.
Baadaye Vatican walishare moja ya picha za tukio hilo katika akaunti yao ya Instagram ikimwonesha mtoto huyo akiwa amekalia kiti cha papa na kuandika ‘A special guest with #popefrancis.
Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis alikuwa akizungumza mbele ya umati mkubwa wa familia mbalimbali zilizohudhuria sherehe za siku ya familia. Baada ya mtoto huyo kupanda jukwaani alienda mbele ya papa na kumtazama na kuzunguka hapa na pale japo hakufanya fujo ya aina yoyote.
Mtoto wa kiume aliyepata utambulisho wa nguo aliyokuwa amevaa ‘the boy in yellow’ alijikuta anachukua ‘attention’ ya waumini wote waliohudhuria siku ya familia St Peter’s Square huko Vatican baada ya kuvamia jukwaani na kukaa na papa Francis kwa muda wa dakika kadhaa. Makadinali walijaribu kutumia njia za kumshawishi kutoka kama kumpatia pipi, lakini mtoto huyo aligoma kuondoka. Papa alimgusa kichwani na kutabasam akamwacha na kuendelea na alichokuwa akikifanya.
Source: Mail Online

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages