Meneja Mauzo na Usambazaji Samsung Tanzania Bw. Sylvester Manyara akiwatambulisha baadhi ya washindi waliojitokeza kupokea zawadi zao kwa waandishi wa habari hawapo pichani katika hafla Maalum ya kuwakabidhi washindi wa droo ya pili ya bahati nasibu ya Pambika na Samsung, jumla ya washindi 15 walipatikana ambao ni wa siku ya Jumatatu hadi Jumapili wiki iliyopita. Wengine pembeni ni Bw. Masenye Chacha, Meneja Uhasibu Samsung Tanzania na Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Abdallah Hemedy
Mshindi wa wiki droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Pambika na Samsung Bw Martin Mwashamwa akikabidhiwa zawadi yake ya jiko la kupashia chakula toka Samsung, pembeki ni Bw Sylvester Manyara
Meneja Mauzo na Usambazaji Samsung Tanzania Bw. Sylvester Manyara akimkabidhi zawadi ya jokofu Muwakilishi wa Bw. Robert David wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi aliyofanyika Quality Center, Dar es Salaam.
Mshindi wa DVD Bw. Hemed Rashid Hemed mkazi wa Dar es Salaam akipokea zawadi kutoka kwa Meneja Mauzo na Usambazaji Samsung Tanzania Bw. Sylvester Manyara katika hafla Maalum iliyofanyika Quality Center Dar es Salaam.
Baadhi ya washindi mbalimbali wa bidhaa toka Samsung katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao na Meneja Mauzo na Usambazaji Samsung Tanzania Bw. Sylvester Manyara katika hafla Maalum iliyofanyika Quality Center Dar es Salaam. Wateja mbalimbali wanaonunu bidhaa za Samsung ndani ya wiki moja kuanzia tarehe 7 Novemba, 2013 mpaka 23 Desemba na kuzisajili, wataingia kwenye droo za kila mwisho wa wiki ambapo washindi watatangazwa jumatatu ya kila wiki, na kwa droo ya mwisho mshindi atatangazwa tarehe 23 Desemba, 2013 na kuondoka na gari mpya aina ya Mitsubishi Double Cabin ikisheheni bidhaa za Samsung.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)