
WAKATI wananchi, ndugu, jamaa na marafiki wakiendelea kuusubiri mwili wa aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba marehemu Dk. Sengodo Mvungi kutoka Afrika Kusini alikopelekwa kwa matibabu, viongozi mbali mbali wameendelea kuzungumzia utashi na ufanyaji kazi wake enzi za uhai wake.
Akizungumza na 100.5 nyumbani kwa Marehemu Kibamba Jijini Dar es Salaam, Mwanadiplomasia ambaye pia ni mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba Dkt.Salim Ahmed Salim, amesema wataikosa michango mingi ambayo alikuwa akiitoa marehemu katika mikutano yao.
Mwili wa marehemu Dr. Mvungi utawasili leo nchini na siku ya Jumamosi kutakuwa na ibada maalum ya marehemu kwenye Kanisa la Mt. Joseph na baadaye mwili wake utaagwa kwenye viwanja vya Karimjee kabla ya Jumapili kusafirishwa kwenda Kisangara Wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi
Mwanzoni mwa mwezi huu Dk Mvungi alivamiwa na kujeruhiwa na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi nyumbani kwake na alhamis iliyopita alisafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi, hadi mauti yalipomfika
Wakati huo huo, RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein hii leo amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba kufuatia kifo cha Dk. Sengondo Mvungi.
Katika salamu zake hizo, Dk. Shein amemuelezea marehemu Dk. Mvungi kuwa ni mzalendo mwenye upendo mkubwa kwa nchi yake, mtaalamu wa sheria na Vilevile mwanasiasa shupavu na makini,hivyo anamchango mkubwa sana katika taita lake.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)