
TIMU ya taifa ya Algeria imepata ushindi wa bao 1-0 iliyouhitaji dhidi ya Burkina Faso katika mchezo uliopigwa jana usiku na kujikatia tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani Brazil.
Waalgeria walipata bao hilo mapema kipindi cha pili, kupitia kwa Madjid Bougherra na kufanya matokeo ya jumla yawe 3-3, baada ya awali Burina kushinda 2-0.
Algeria inaungana na Cameroon, Ivory Coast, Ghana na Nigeria kukamilisha idadi ya timu tano za Afrika.
Burkina Faso, washindi wa pili wa Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu, walikuwa wakipigania kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.

Katika mchezo uliopigwa mapema jana, timu ya taifa ya Ghana, imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil, licha ya kufungwa mabao 2-1 na Misri katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa jeshi mjini Cairo.
Ghana imefuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 7-3, baada ya kufanya kazi nzuri katika mchezo wa kwanza mjini Kumasi mwezi uliopita na sasa watakwenda Brazil kujaribu kuendeleza mafanikio ya fainali zilizopita Afrika Kusini mwaka 2010 walipofika Robo Fainali.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)