KINANA AWASILI VWAWA WILAYANI MBOZI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KINANA AWASILI VWAWA WILAYANI MBOZI

 1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh Abbas Kandoro mara baada ya kuwasili katika ofisi za chama hicho mjini Vwawa Wilaya ya Mbozi asubuhi hii akitokea wilaya ya Momba katika ziara yake ya kikazi ya mikoa mitatu Ruvuma, Mbeya na Njombe, Kinana ameongozana na ujumbe wake akiwa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
2Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro mara baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ku wasili mjini Vwawa wilayani Mbozi asubuhi hii, kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi 3Baadhi ya wana CCM wakishiriki kucheza ngoma na kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 5Baadhi ya machifu wa Mbozi wakisubiri kusalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
6Baadhi ya viongozi mbalimbali na wananchi wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili wilayani Mbozi. 8Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na mbunge wa jimbo la Mbozi mashariki Ndugu Godfrey Zambi akisalimiana na wana CCM wakati wa mapokezi hayo 9 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na machifu 10Wana CCM wakiwa katika mapokezi hayo 11 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma ya asili ya wanyiha iliyokuwa ikitumbuizwa katika mapokezi hayo.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MBOZI 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages