DJ Rankim Ramadhan enzi za uhai wake.
Taarifa zilizotufikia muda mchache uliopita jiloni hii zinasema kuwa DJ mkongwe nchini Rankim Ramadhan, amefariki dunia wakati akifanyiwa upasuaji Hospitali ya Mwananyama.
Ujumbe wa mwisho wa Novemba 4 mwaka huu alioutoa DJ Rankim katika ukurasa wake wa Facebook unanukuu maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Rankim Ramadhani "Madokta wanasema ni apendix ndiyo inayonisumbua hapa sijala toka jana maumivu tu ndiyo yananitesa tumbo na mbavu vinauma sana na ss hv nachoma kristapen ya tatu kwa leo but theres no releaf"
Mipango ya mazishi inaweza kuwa Sinza kwa Remmy au Salasala.
LUKAZA BLOG INAPENDA KUTOA POLE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KWA KUONDOKEWA NA KIPENZI CHETU NA MUNGU AWATIE NGUVU NA KUWAPA UWEPESI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU .AMEN






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)