BONDIA KALAMA NYILAWILA AWAASA MABONDIA KUACHA USHIRIKINA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BONDIA KALAMA NYILAWILA AWAASA MABONDIA KUACHA USHIRIKINA

 BONDIA Kalama Nyilawila 

BONDIA  Karama Nyilawila amewataka mabondia wa Tanzania kuacha imani za kishirikina na badala yake wafanye mazoezi  ili waweze kufikia mafanikio. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nyilawila alisema  hapendezwi na vitendo hivyo kwani vinauwa viwango vya michezo nchini. Alisema mabondia wanatakiwa wasiamini kabisa na kwamba wamekuwa wakifanya mambo hayo wanapoenda kupambana nje ya nchi. Nawasihi waachane na imani za kishirikina kwani wanapokwenda huko huishia kupigwa kwa KO ila naamini wakizingatia mazoezi yatawasaidia kufanya vema,"alisema.

Alisema mazoezi pekee ndiyo yatakayomsaidia bondia kushinda pambano lake na si kwenda kwa mganga na kumpa nguvu za giza na badala yake jitihada zake binafsi  ulingoni ndizo zitakazomfaa. Alisema watu wasitafute mchawi aliyesababisha Tanzania isifanye vema kimataifa kwani wachawi ni wanamichezo wenyewe na wengi wamekuwa wakiamini imani hizo.

Nyilawila alisema kwa sasa yupo katika mazoezi makali chini ya meneja wake Seleman Zugo na kwamba  amejipanga kushinda mapambano yake yote yaliyopo mbele yake kwa KO raundi za mwanzoni ambambo hivi karibuni bondia huyo alimshinda kwa K,O  ya raundi ya kwanza bondia Kaminja Ramadhani mpambano ulioandaliwa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi  Rajabu Mhamila 'Super D' uliofanyika NOVEMBA 10 katika ukumbi wa Zulu Paradise pugu kilumba

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages