ASKARI WA OPARESHENI YA KUWASAKA MAJANGIRI WAKIONGOZWA NA JESHI LA WANANCHI TANZANIA (JWTZ) LAWAMANI KWA KUCHOMA NYUMBA YA 600 ZA WANAKIJIJI NA KUWAACHA BILA MAKAZI MKOANI KATAVI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ASKARI WA OPARESHENI YA KUWASAKA MAJANGIRI WAKIONGOZWA NA JESHI LA WANANCHI TANZANIA (JWTZ) LAWAMANI KWA KUCHOMA NYUMBA YA 600 ZA WANAKIJIJI NA KUWAACHA BILA MAKAZI MKOANI KATAVI

Hapa ndipo wanapoishi watu hawa baada ya nyumba zao kuchomwa moto
Watoto wakiwa michezoni huku wasijue watalala wapi ukifika usiku
Ni majonzi makubwa
Hizi ndizo nyumba zao , wanalala chini ya miti baada ya nyumba zao kuchomwa moto 
Wakazi wa kijiji cha kabage wakihama kijiji hicho baada ya nyumba zao  kuchomwa na askari waliokuwa wanafanya oparesheni ya kuwasaka majangili  nyumba hizo zilichomwa wiki iliyopita kijijini hapo na kusababisha  maelfu ya wanakijiji kuishi chini ya miti
Mzee na binti yake wakiwa wanaondoka wanaondoka 
Wakina mama wakiwa wanafungasha 
Wakubwa kwa watoto wakiwa wanakihama kijiji hicho 
Wakiendelea kuhama kijijini hapo 
Wakazi wa kijiji cha Kabage wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa  wanaishi chini ya miti na familia zao baada ya nyumba zao kuchomwa moto  na askari waliokuwa wanafanya oparesheni majangiri wiki iliyopita jumla  ya zaidi ya kaya 500 zilichomewa nyumba kijijini hapo na kuleta  malalamiko ya wanakijiji hao kwa kile wanachodai kijiji hicho ni halali  na kimesajiliwa kisheria toka mwaka jana na kupewa usajili wenye namba  KT/KIJ/47
Hawana makazi tena hawa 
Mtoto akiwa amelala huku akiwa hana pa kuhifadhiwa ikiwa nyumba yao imechomwa moto 
Mchungaji wa kanisa la PAG wa kijiji  cha Mwamkulu Petro Mahenga akimfariji mmoja wa wahanga waliochomewa  nyumba zao katika kijiji cha kabage wilayani Mpanda Daudi Belehiwa ambae pia mke wake aitwae Kurwa Elias alijifungua mtoto ambae hajatimiza miezi yake kutokana na kutembea kwa muda mrefu wakati akiwakimbia askari hao hata hivyo mtoto huyo aliezaliwa akiwa na miezi nane alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Vyombo vikiwa havina pa kupelekwa 
Dogo akiwa ameishiwa Nguvu 
 Inasikitisha sana Wanakijiji hawa hawana makazi sasa 

Na Walter Mguluchuma-Katavi yetu Mpanda

Askari waliokuwa wanafanya operesheni ya kuwasaka  
majangili waliokuwa wakiongozwa na JWTZ  wamelalamikiwa kwa kuchoma  
nyumba za wanakijiji cha Kabage Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi na 
kuwasababishia wananchi wa kijiji hicho kuishi chini ya miti na 
akina mama kujifungua kabla ya wakati


Mwenyekiti wa Kijiji hicho Maganga Kasope alisema tukio  
hilo lilitokea hapo Oktoba 28 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi na  
kusababisha zaidi ya kaya mia sita kukosa makazi ya kuishi


Alisema kijiji hicho chenye wakazi zaidi ya elfu kumi ni 
kijiji halali kwani kalisajiliwa  toka mwaka jana na kupewa usajiri  
wenye namba za usajiri wa kijiji KT/KIJ/47 hivyo wameshangazwa na wakazi 
wa kijiji hicho kuchomewa nyumba zao wakati ni kijiji halali 

alisema kuwa katika tukio hilo akina mama watatu ambao walikua wajawazito walilazimika kujifungulia kwenye mbuga za mpunga  
wakati wakikimbia kuelekea kijiji cha jirani cha mwamkulu kujihifadhi  
hivyo kutokana kutembea kwa umbali mrefu hivyo ililazimika kujifungulia  
njiani na kujifungua watoto wakiwa salama


Kwa upande wake mhanga wa tukio hilo  Daudi  Lulehiwa 28  alisema kutokana na tukio hilo iliwalazimu ketembea umbali mrefu kwa ajiri ya kukimbilia  katika kijiji cha jirani cha Mwamkulu huku wakiwa wamebeba mizigo yao na iliwalaziri hata watoto wao wadogo kutembea kwa miguu umbali huo mrefu


Alisema mkewe aitwaye Kulwa Elias 24 ambae alikuwa ni  mjamzito wa miezi minane  kutokana na kutembea umbali huu huku akiwa amebeba mizigo  aliweza kujifungua mtoto wa wakike  ambae alikuwa sio ridhiki na alifariki muda mfupi baada ya kujifungulia chini ya mti


Nae mchungaji wa Kanisa la wa Kanisa la P.A.G wa Kijiji  
cha Mwamkulu Mchungaji Petro  Mahega  alisema toka wahanga hao  
waliokimbilia kijijini hapo wamekuwa wakiishi kama wanyama wao na  
familia zao


Alieleza kutokana na wahanga hao kuishi chini ya miti na 
mbaya zaidi hapo juzi walinyeshewa na mvua ambayo ilinyesha majira ya  
usiku hivyo ametowa jengo la Kanisa lake igawa ni dogo sana litumike kwa 
ajiri ya kuwahifadhi wahanga hao


Kwa 
upande wake mhanga mwingine Malidadi Gwachele 72 ambae anaishi na  
familia yake ya watu 20 wakiwa chini ya mtu alieleza kuwa  wameanza  
kuhathirika kwa kupata magonjwa ya kuharisha


Alisema hari hiyo imesababishwa na maji wanayo kunywa na 
mazingira wanayoishi na hasa watoto wadogo ndio wanao athirika zaidi
za magonjwa hayo 
Mdae 
Masanja  alisema mbali ya kuchomewa nyumba yake pia amepoteza chakula  
chake ambacho kiliteketea kwa moto baada ya kushindwa kukihamisha kwenye 
nyumba yake wakati ikiungua


Alisema sasa hivi wanalala nje bila hata kujali jinsia  
za familia walizo nazo kutokana natukio lenyewe inawalazimu walale hivyo 
na wamekuwa wakijisaidia kwenye vichaka


Aidha Mhanga Katali Ngeleja  alieleza mbele ya mwandishi 
wa habari hizi ambae alitembelea eneo hilo kuwa wako watoto wenye umri 
kati ya miaka saba na nane  walipotezana na familia zao kwa muda wa siku 
mbili 


Alieleza yupo pia mwenzao mmoja ambae alikuwa anamiliki  
mashine ya kusanga unga iliteketea kabisa kwa moto ikiwa ndani ya  
kibanda cha nyumba 
HABARI NA PICHA NA KATAVI YETU BLOG

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages